Historia
Fupi ya Kwaya ya Mamajusi Moshi
Kwaya
hii ilianzishwa mnamo mwaka 1975 tarehe 11.10.1975, siku ya
Jumapili saa 10:00 chini ya uongozi wa Mchungaji Kiongozi Majengo
Moshi Rev. Godwin Katoto. Ilikuwa na jumla ya wanakwaya 18 wanawake
na wanaume; na ikaitwa kwaya ya Uinjilisti ya Kianglikana Majengo
Moshi.
Mnamo
mwaka 1979 kwaya ilikwenda kurekodi kwa mara ya kwanza kule Radio
Habari Maalum, Maragu - Moshi kabla ya studio kuhamishwa Arusha.
Mnamo
mwaka 1980, kwaya hii ilikwenda Mvumi, Dodoma kwenye tamasha la
uimbaji wa Dayosisi wakati huo ikiwa chini ya Diocese of Central
Tanganyika (DODOMA D.C.T.). Pia walirekodi tena mara ya
pili kwenye studio ya msalato, Dodoma mwaka huo. Vipindi vyote
hivyo kwaya ilikuwa chini ya mwimbaji mwanzilishi ndugu Joseph
Semaghembe ambaye pamoja na kuanzisha kwaya, bado yu mwimbaji
hadi leo.
Mnamo
mwaka 1982 na 1983, kwaya hii iliingia Studio ya Sauti ya Injili
Moshi, na kurekodi matoleo mawili; ikiwa chini ya jina jipya:
MAMAJISU KWAYA MAJENGO - MOSHI. Jina hili jipya lilizaliwa
mwaka 1982 na maana ya jina hili ni - Wafalme (Mamajusi) wa Mashariki
waliyoongozwa na nyota kutoka Mashariki kwenda kumwona mtoto aliyezaliwa;
Mkombozo Yesu Kristo (Mathayo 2:1-6).
Pamoja
na kwaya kurekodi matoleo yaliyotajwa hapo juu, manne hayakuweza
kusambazwa au kutolewa kibiashara ili kujitangaza kiinjili kwa
njia ya nyimbo. Matoleo ambayo kwaya inamiliki ni haya yafuatayo:
1 |
Ee
Mungu Unirehemu |
1997 |
2 |
Jee
Huu Ni Wakati |
1998 |
3 |
Bwana
Ni Wa Ajabu |
1999 |
4 |
Hey
Haleluya |
2000 |
5 |
Homa
Ya Dunia |
2001 |
Pia
kwaya inatoleo la kwanza linalomilikiwa na Radio Habari Maalum,
Arusha linaloitwa MUNGU KAUMBA.
Kwaya
hii kwa sasa ina jumla ya wanakwaya sitini tu (60) na kwa sasa
inamilikiwa na wakristo wa Kanisa la Kianglikana Majengo Moshi
chini ya Dayosisi mpya ya mlima Kilimanjaro (Arusha DMK).
|