QUICK QUIZ


1) Jina lake mkewe mfalme Sauli aliitwa nani? (1Sam 14:50).
a) Ahinoamu
b) Merabu
c) Mikali
d) Abigaili.

2) "Ndipo mkewe akamwambia, Je! Wewe hata sasa washikamana na utimilifi wako? Umkufuru Mungu ufe.." Huyu alikuwa mke wa nani?
a) Mkewe Suleimani
b) Mkewe Daudi
c) Mkewe Ayubu
d) Mkewe Yoeli

3)Ni watu wepi wawili Biblia inasema hawakufa?
a) Eliya and Elisha
b) Elisha and Henoko
c) Henoko and Eliya
d) Eliya and Musa

4) Lakini pasipo imani ____________ kumpendeza; kwa maana amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.. (Hbr 11:6)
a) ni utupu
b) inahitajika
c) haiwezekani
d) haiepukiki

5) Basi Israeli akampenda Yusufu kuliko wanawe wote, maana ni mwana wa uzee wake, akamfanyia kanzu ndefu.(Mwanzo 37:3). Mama yake Yusufu aliitwa nani?
a) Lea
b) Raheli
c) Hana
d) Sara

6 Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kwa jinsi zao, na kila ndege arukaye, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. (Mwanzo 1:21). Hii ilikuwa ni siku ya ngapi?
a) Siku ya pili
b) Siku ya tatu
c) Siku ya nne
d) Siku ya tano

7) Kulingana na Mambo ya Walawi, uhai wa wanyama wote upo wapi? (Walawi 17:14)
a) Katika pumzi yao
b) Katika mioyo yao
c) Katika damu yao
d) Katika nafsi zao

8) Samson alikamata mbweha wangapi kisha akatwaa vienge vya moto akawafunga mkia kwa mkia, akatia kienge kati ya kila mikia miwili? (Waamuzi 15:4-5).
a) 57
b) 34
c) 300
d) 500

9) "... Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza huko ____________." (Matendo ya Mitume 11:26)
a) Dameski
b) Korintho
c) Antiokia
d) Efeso

10) Hao wana wa Benyamini walihesabiwa siku ile kutoka ile miji, watu waume ishirini na sita elfu waliotumia upanga, zaidi ya hao waliokaa Gibea, ambao walihesabiwa watu wateule mia saba. Katika watu hao wote walikuwako watu waume ________ waliochaguliwa, wenye shoto; kila mmoja alikuwa anaweza kuutupia unywele mawe kwa teo, wala asikose. (Waamuzi 20:15-16)
a) 700
b) 733
c) 20,000
c) 23, 400